MWANDISHI JELA MIAKA KUMI NA FAINI KWA KURIPOTI UGAIDI

April 25, 2017




hakam.org


Mahakama ya Kijeshi Nchini Cameroon imemtia hatiani mwandishi mmoja wa Radio France Kimataifa AHMED ABBA kwa  kuriporti kuhusu Kikundi Cha kigaidi (BOKO HARAM).
Kwa mujibu wa mahakama hiyo mwanadishi huyo ameripoti habari za "kushabikia vitendo vya ugadi" lakini pia amehusika"kutakatisha fedha" zianzotumika kwa vitendo vya kigaidi kinyume na sheria ya kupinga ugaidi ya mwaaka 2004.

Kwamujibu wa sheria hiyo ya kameruni ya kupambana na Vitendo Vya Kigaidi ya 2014 pamoja na makosa mengine  kutakatisha fedha zinazotumika katika vitendo hivyo ni kosa ambalo adhabu yake ni hukumu ya kifo.
Hata hivyo mwandishi huyo amepewa dhabu ya kifungo cha miaka 10 pamoja na faini.




Hatahivyo  shirika la kutetea haki za binadam la AMNESTY INTERNATIONAL limeonesha kuto kukubaliana na mwenendo mzima wa mashitaka na hukumu iliyotolewa.
 

You Might Also Like

0 comments