KUFUKUZWA BOSI UNDP: MADHARA YA KISHERIA.

April 26, 2017


Tuanzie kwa kujibu hili swali hapo juu.
Nchi husika inaweza kujihusisha na masuala ya kidiplomasia kama kukaribisha mabalozi au kuwakataa lakini pia kumuondoa balozi yeyote nchini bila kutoa maelezo yeyote kwakumtangaza kuwa "persona non grata" yaani maneno ya kilatini ambayo kiswahili chake ni "mtu asiye takiwa".

kitendo hiki kinaruhusiwa kwa mujibu wa MKATABA WA VIENA JUU YA UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA (Viena Convention On Diplomatic Relations 1961) ibara ya 9.

lakini tofauti na mabalozi ambao wana wakilisha nchi zao, Viongozi wa UN ni waajiriwa wa katibu mkuu wa umoja huo hivyo sheria hii inayo weza kum "declare" mtu "persona non grata" haifanyi kazi hapa.hivyo uamuzi wa kumfukuza mwajiriwa wa UN haufanyiki kwa upande mmoja ni ukiukwaji wa taratibu na serikali ilifaa kuwashirikisha mabosi zake, Kama inavyo elezewa na mwandishi August Reinisch








 Ni hayo tuu kwa leo #IDHAAYASHERIA



You Might Also Like

0 comments