NDOA ZA UTOTONI MALAWI BASI

April 28, 2017




chikaoduablog
 Baada ya raisi wa nchi hiyo kusaini muswada wa mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo wiki hii ndoa hizo sasa basi.Muswada huo umelenga kupandisha umri wa kisheria wa ndoa kuwa miaka 18.

 Malawi has become the latest African country to outlaw child marriage. #IDHAAYASHERIA https://t.co/htaHhzUKus pic.twitter.com/BKIWkMQZ6M
Tatizo la ndoa za utotoni limekithiri katika nchi nyingi za kiafrika ambapo licha ya kuchangiwa na mila na deturi za kiafrika lakini pia sheria za ndoa  zimekuwa na mikanganyiko mingi kuhusiana na upi ni umri sahihi wa kuoa au kuolewa. Mfano mzuri ni sheria ya ndoa ya Tanzania ya mwaka 1971 ambayo ina tamka wazi kuwa umri wa msichana kuolewa ni miaka 15.sheria hii ambayo imetajwa na mahakama kuu Tanzania kuwa ya kibaguzi hususani kwa wasichana ni moja kati ya sheria nyingi zinazo changia uwapo wa ndoa za utotoni, jambo ambalo limezua mijadala mikubwa sana kutoka Asasi mbali mbali zisizo za kiserikali lakini pia Miongoni mwa wabunge watanzania wakisema kuwa ni wakati mwafaka sheria hii ifanyiwe marekebisho stahiki kwani umri huo ni mdogo sana na pia una mkandamiza mtoto wakike.



#IDHAAYASHERIA
 

You Might Also Like

0 comments